عربي - Arabic English Qafár af - Afar Afrikaans - Afrikanns Akan Shqip - Albanian አማርኛ - Amharic Հայերեն - Armenian অসমীয়া - Assamese Azərbaycanca - Azerbaijani Bamanankan - Bambara Bassa Bemba বাংলা - Bengali Bosanski - Bosnian Български - Bulgarian မြန်မာဘာသာ - Burmese Bisaya - Cebuano Cham Нохчий - Chechen chiCheŵa - Chewa 中文 - Chinese Адыгэбзэ - Circassian Hrvatski - Croatian Česky - Czech Dagbani Dansk - Danish فارسی دری - Dari Dendi ދިވެހި ބަސް - Dhivehi Nederlands - Dutch إستوني - Estonian Suomi - Finnish Français - French Fulfulde - Fula ქართული - Georgian Deutsch - German Ελληνικά - Greek ગુજરાતી - Gujrati Kreyòl ayisyen - Haitian Creole Hausa हिन्दी - Hindi Magyar - Hungarian Igbo Indonesia - Indonesian Italiano - Italian 日本語 - Japanese Jóola - Jola ಕನ್ನಡ - Kannada Қазақша - Kazakh ភាសាខ្មែរ - Khmer Kikuyu Ikinyarwanda - Kinyarwanda Ikirundi - Kirundi 한국어 - Korean كوردی سۆرانی - kurdish كوردي kurmancî - Kurmanji Kyrgyz ລາວ - Lao latviešu - Latvian Lingala lietuvių - Lithuanian Luganda Македонски - Macedonian Maguindanaon Malagasy - Malagasy Bahasa Melayu - Malay മലയാളം - Malayalam Mandinka मराठी - Marathi Mõõré - Moore नेपाली - Nepali أنكو - NKo Norwegian ଓଡ଼ିଆ - Odia oromoo - Oromo پښتو - Pashto فارسی - Persian Polski - Polish Portuguese ਪੰਜਾਬੀ - Punjabi Română - Romanian Русский - Russian Српски - Serbian Shona සිංහල - Sinhala Slovenščina - Slovenian Soomaaliga - Somali Soninke Sesotho - Sotho Español - Spanish Kiswahili - Swahili Svenska - Swedish Tagalog Тоҷикӣ - Tajik தமிழ் - Tamil తెలుగు - Telugu ไทย - Thai ትግረኛ - Tigrinya Türkçe - Turkish Ukrainian اردو - Urdu ئۇيغۇرچە - Uyghur Ўзбек - Uzbek Việt Nam - Vietnamese Wolof Yao Yorùbá - Yoruba Zarma زولو - Zulu
839 Hadithi
Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii
Makundi
Daraja la hadithi
Imesimuliwa katika
Onyesha vyanzo vilivyobaki
Msimulizi
Onyesha wasimulizi wote (57)
Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Abuu Aamir, amesema Naafii: Nafikiri ni Hafswa -Yakuwa aliulizwa kuhusu kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hakika nyinyi hamkiwezi, akasema: Akaambiwa hebu tueleze. Akasema: Akasoma kisomo cha taratibu, akasema Abuu Aamiri: Akasema Naafii: Akatusimulia Abuu Mulaika: "Alhamdulillaah Rabbil-Aalamiin" [Al-Faatiha: 1] Kisha akakata "Al Rahmaanir Rahiim" [Faatiha:3] kisha akakata "Maaliki yaumid diin".
Sahihi Imepokelewa na Ahmad
"Atakayeacha Ijumaa tatu kwa kuzipuuzia; Mwenyezi Mungu hupiga muhuri katika moyo wake"
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
"Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika mkono wake, na akasema: "Ewe Muadhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda", Akasema: "Ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Nasai na Ahmad
"Kusimzuie mmoja wenu kuwaogopa watu akaache kusema haki atakapoiona au kuijua".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba.
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na Ahmad
"Muumini iliyekamilika zaidi imani yake ni yule mwenye tabia nzuri zaidi kuliko wengine, na mbora wenu ni yule mbora wenu kwa wake zake".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Hakuwahi kuwapiga vita Mtume rehema na amani ziwe juu yake watu hata siku moja isipokuwa kwanza alianza kuwaita katika Uislamu.
Sahihi Imepokelewa na Ahmad na Albayhaqy