Skip to content

Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda

Kutoka kwa Abul Abbasi Sahli bin Sa'di As-saai'diy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nijulishe amali ambayo nikiifanya atanipenda Mwenyezi Mungu na watu watanipenda, akasema:

"Ipe nyongo dunia Allah atakupenda ,na usivitolee macho vitu vya watu, watu watakupenda".

«ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ، وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النَّاسُ».

Imepokelewa na Ibn Majah na wengineo kwa sanadi nzuri.
Amesema Imamu Nawawi: Hadithi hii ni hasan
Ufafanuzi

Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali ambayo akiifanya Mwenyezi Mungu atampenda na watu watampenda, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Atakupenda Mwenyezi Mungu utakapoacha yasiyo na msingi katika Dunia, na yale yasiyokunufaisha katika Akhera, na ukaacha yale yanayoweza kuwa na madhara katika dini yako, na watu watakupenda utakapoyapa nyongo yaliyoko mikononi mwao miongoni mwa vitu vya kidunia; kwa sababu wanayapenda kulingana na tabia zao za asili, na atakayebanana nao katika hayo watamchukia, na atakayewaachia watampenda.

Katika Faida za Hadithi

Ubora wa kuipa nyongo dunia, nayo: Ni mtu kuacha yasiyofaa katika Akhera.

Kuipa nyongo dunia daraja yake ni kubwa kuliko unyenyekevu; kwa sababu unyenyekevu ni kuacha mambo ambayo huenda yakakudhuru, na kuipa nyongo dunia ni kuacha yasiyofaa katika Akhera.

Amesema Assanadi: Hakika Dunia inapendeka kwa watu, yeyote atakayepambana nao humo atachukiza kwao kwa kadiri ya hilo, na atakayewaacha na hicho wanachokipenda atapendeka ndani ya nyoyo zao kwa kiwango cha hilo.

Rejea

Sunanu Ibn Maajah (5/ 225) (4102).

Zaidi (7)

Al-Arbauna An-Nawawiyah (ص118) (ح31).

التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص73).

فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين (ص111).

الفوائد المستنبطة من الأربعين النووية.

للشيخ عبد الرحمن البراك (ص87).

الأحاديث الأربعون النووية وعليها الشرح الموجز المفيد.

لعبد الله بن صالح المحسن (1/61).