Skip to content

Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

"Hakuna kitu kinachotukuzwa zaidi kwa Allah Mtukufu kuliko dua".

«لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللهِ تَعَالَى مِنَ الدُّعَاءِ».

Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Ni nzuri (Hasan)
Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna chochote katika ibada kilicho bora zaidi mbele ya Allah Mtukufu kuliko dua; kwa sababu ndani yake kuna kukiri utajiri wa Allah Mtukufu, na kukiri kushindwa kwa mja na kuhitajia kwake kutoka kwake.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Ubora wa dua nakuwa mwenye kumuomba Allah basi huwa kamtukuza, na amekiri kuwa Yeye ni mkwasi -Aliyetakasika- kwani Masikini haombwi, nakuwa Yeye ni Msikivu, kwani kiziwi haombwi, nakuwa Yeye ni mkarimu, kwani bahili haombwi, nakuwa yeye anahuruma, kwani mkorofi haombwi, nakuwa Yeye anaweza, kwani asiyejiweza haombwi, nakuwa Yeye yuko karibu, kwani aliyembali hasikii, na zinginezo katika sifa za utukufu na za uzuri wa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na Kutukuka-.

Rejea

Sunanu Tirmidhiy (5/ 385) (3370).

Sunanu Ibn Maajah (5/ 6) (3829).

Musnad wa Ahmad (14/ 360) (8748).

Zaidi (8)

توضيح الأحكام من بلوغ المرام.

للبسام (7/ 546).

منحة العلام في شرح بلوغ المرام.

لعبد الله الفوزان (10/ 416).

فتح ذي الجلال والإكرام.

لابن عثيمين (6/ 481).

سبل السلام بشرح بلوغ المرام.

للصنعاني (2/ 707).