Skip to content

Itakapokimiwa swala basi hakuna swala nyingine isipokuwa swala ya faradhi

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

"Itakapokimiwa swala basi hakuna swala nyingine isipokuwa swala ya faradhi".

«إِذَا أُقِيمَتِ الصَّلَاةُ فَلَا صَلَاةَ إلَّا المَكْتُوبَةُ».

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemkataza atakayekuwa msikitini aanze kuswali sunna baada ya kukimiwa swala ya faradhi.

Katika Faida za Hadithi

Katazo la kuswali sala ya sunna itakapokimiwa swala ya faradhi msikitini.

Katazo la kuanza sunna baada ya kukimiwa swala, sawa sawa iwe ni sunna yenye utaratibu maalumu kama sunna ya Alfajiri na Adhuhuri au nyingineyo.

Pindi itakapokimiwa swala akiwa ndani ya sala ya sunna; ikiwa amebakiza kiasi kidogo chini ya rakaa moja basi ataikamilisha kwa haraka, na isipowezekana basi ataikatisha ili aipate takbira ya kuanza swala.

Rejea

Swahiih Muslim (1/ 493) (710).

Zaidi (1)

البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (15/ 246).