Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Hakuwahi kuswali tena Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala yoyote baada kuteremka kwake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" [An-Naswir:1] Isipokuwa alikuwa akisema ndani yake: "Sub-haanaka Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii, (umetakasika Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, ewe Mwenyezi Mungu nisamehe)". Na kutoka kwa Aisha amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akikithirisha kusema katika rukuu yake na sijida yake: "Sub-haanaka llaahumma Rabbanaa wabihamdika Allaahummagh-firlii" Umetakasika ewe Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi, na sifa njema ni zako, ewe Mola wangu Mlezi nisamehe" Akiifasiri Qur'ani.
مَا صَلَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلاَةً بَعْدَ أَنْ نَزَلَتْ عَلَيْهِ: {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالفَتْحُ} [النصر: 1] إِلَّا يَقُولُ فِيهَا: «سُبْحَانَكَ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي». وعَنْها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ فِي رُكُوعِهِ وَسُجُودِهِ: «سُبْحَانَكَ اللهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللهُمَّ اغْفِرْ لِي» يَتَأَوَّلُ الْقُرْآنَ.
Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipoteremshiwa juu yake: "Itakapokuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ufunguzi" Akaifasiri Qur'ani na akaanza kuitekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kauli yake: "Basi zitakase sifa za Mola wako Mlezi na umuombe msamaha", akawa akikithirisha kusema katika rukuu zake na sijida zake wakati wa swala: "Umetakasika" Na ni kukutakasa wewe dhidi ya kila mapungufu yale yasiyokufaa, "Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako" Kwa sifa nzuri kwako kwa ukamilifu wa dhati yako na sifa zako na matendo yako, "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe" na zifute kwangu dhambi zangu, na uziachilie mbali.
Kupendeza kukithirisha dua hii katika rukuu na sijida.
Kuomba msamaha mwisho wa umri kuna angalizo la kuhitimisha ibada zote namna hiyo, na hasa hasa swala kwa kuomba msamaha, ili azibe yale yaliyojitokeza ndani yake miongoni mwa mapungufu.
Jambo zuri linalotumika kukubaliwa dua kupitia jambo hilo ni kutaja mazuri yake na sifa zake, na kumtakasa dhidi ya mapungufu na aibu.
Fadhila ya kuomba msamaha, na kuutafuta katika kila hali.
Ukamilifu wa utumwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kutekeleza kwake amri ya Mwenyezi Mungu.
Swahiih Al Bukhaariy (6/ 178) (4968.
4967).
Swahiih Muslim (1/ 350-351) (484).
Zaidi (10)
تيسير العلام.
للبسام (ص214).
تنبيه الأفهام.
للعثيمين (2/ 278).
الإفهام في شرح عمدة الأحكام.
لابن باز (ص263).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام.
لإسماعيل الأنصاري (1/ 176).
خلاصة الكلام.
فيصل المبارك (ص97).
Imenukuliwa katika vitabu
16 VitabuZaidi (15)
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"سبحانك اللهم ربنا وبحمدك اللهم اغفر لي".
- الذكر والدعاء والعلاج بالرقي من الكتاب والسنة"سبحانك اللهم ربنا وبحمدك، اللهم اغفر لي".
- تطبيق القرآن والأذكارأذكار الصلاة((سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي))[58].
- تطبيق القرآن والأذكارأذكار الصلاة((سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي)) [66].
- حصن المسلم من أذكار الكتاب والسنةحصن المسلم«سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي»[58].
- حصن المسلم من أذكار الكتاب والسنةحصن المسلمسُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي
- حصن المسلم من أذكار الكتاب والسنةحصن المسلم«سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي» [66].
- حصن المسلم من أذكار الكتاب والسنةحصن المسلمسُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي
- رسالة في الأذكار1كان النبي صلى الله عليه وسلم يُكْثِرُ أن يقول في ركوعه وسجوده: «سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي» يَتأوَّلُ القرآن.
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 1 «سبحانك اللهم ربنا وبحمدك، اللهم اغفر لي».
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 7«سبحانكَ اللّهم ربَّنَا وبحمدِكَ، اللّهم اغْفرْ لي».
- صلاتنا الخاشعة"سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي" ([22])
- من الأحكام الفقهية في الطهارة والصلاة والجنائز«سُبْحَانَكَ الْلَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، الْلَّهُمَّ اغْفِرْ لِي» [38]،
- من الأحكام الفقهية في الطهارة والصلاة والجنائز«سُبْحَانَكَ الْلَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، الْلَّهُمَّ اغْفِرْ لِي» [42]،
- موسوعة الأسئلة (المجموعة الأولى)«سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي»