Skip to content

Hivi sikutumi katika yale aliyonituma kwayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-? (Nenda) Kamwe usiache sanamu au picha ila uifute, wala kaburi refu kupita kiasi isipokuwa umelisawazisha

Kutoka kwa Abul Hayyaji A-Asady amesema:

Ally bin Abii Twalib alisema kuniambia: Hivi sikutumi katika yale aliyonituma kwayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-? (Nenda) Kamwe usiache sanamu au picha ila uifute, wala kaburi refu kupita kiasi isipokuwa umelisawazisha.

قَالَ لِي ‌عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ: أَلَا أَبْعَثُكَ عَلَى مَا بَعَثَنِي عَلَيْهِ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ أَنْ لَا تَدَعَ تِمْثَالًا إِلَّا طَمَسْتَهُ، وَلَا قَبْرًا مُشْرِفًا إِلَّا سَوَّيْتَهُ.

Imepokelewa Imamu Muslim
Sahihi
Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwatuma Masahaba wake wasiache "Sanamu" nayo ni picha ya kiumbe hai yenye kiwiliwili- isipokuwa wameliondoa au kuifuta. Na wasiache kaburi lililonyanyuka ila wamelisawazisha na ardhi, na wayabomoe yaliyomo katika majengo, au walisawazishe lisinyanyuliwe sana kupita usawa wa ardhi, bali linyanyuliwe kiasi cha shibri moja (kipimo cha kiganja).

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Uharamu wa kuvipiga picha viumbe hai; kwa sababu hilo ni njia za kuelekea katika ushirikina.

Sheria ya kuondoa uovu kwa mkono kwa mwenye mamlaka au uwezo wa hilo.

Pupa ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuondoa mambo yote ambayo yana alama za enzi za ujinga, kama picha na vinyago na majengo yaliyo juu ya makaburi.

Rejea

Swahiih Muslim (2/ 666) (969).

Zaidi (8)

القول المفيد على كتاب التوحيد.

لابن عثيمين (2/ 446).

الملخص في شرح كتاب التوحيد.

لصالح الفوزان (ص402).

الجديد في شرح كتاب التوحيد.

لمحمد القرعاوي (ص447).

كتاب التوحيد.

للإمام محمد بن عبد الوهاب (ص138).