Skip to content

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunaiona Jihadi kuwa ni amali bora zaidi, basi je tupigane? Akasema: "Hapana, lakini Jihadi iliyo bora zaidi ni Hija iliyokubaliwa."

يَا رَسُولَ اللَّهِ، نَرَى الجِهَادَ أَفْضَلَ العَمَلِ، أَفَلاَ نُجَاهِدُ؟ قَالَ: «لَا، لَكُنَّ أَفْضَلُ الجِهَادِ: حَجٌّ مَبْرُورٌ».

Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Sahihi
Ufafanuzi

Maswahaba Mwenyezi Mungu awawie radhi, waliona Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kupigana na maadui kuwa ni matendo bora, Basi Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akamuuliza Mtume Rehema na Amani zimshukie, je nao wapigane Jihadi? Basi rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, akawaelekeza kwenye Jihadi bora zaidi kwao, ambayo ni Hija iliyokubalika kwa mujibu wa Qur’ani na Sunna, isiyo na dhambi na unafiki (Riyaa).

Katika Faida za Hadithi

Jihadi ni katika amali bora kwa wanaume.

Haji kwa wanawake ni bora kuliko Jihadi, na ni miongoni mwa matendo bora kwao.

Amali zinazidiana ubora na zinatofautiana kulingana na mfanyaji.

Hija inaitwa Jihad; Kwa sababu ni Jihadi kwa ajili ya nafsi, na inahusisha kutoa mali na nguvu ya mwili, hivyo ni ibada ya mwili na mali kama kupigana Jihadi kwa ajili ya Allah.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (2/ 133) (1520).

Zaidi (6)

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (2/ 402).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمصطفى الخِن وغيره (2/ 902).

شرح رياض الصالحين.

لابن عثيمين (5/ 321).