Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Marthad Al-Anawiy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea".
«لَا تَجْلِسُوا عَلَى الْقُبُورِ، وَلَا تُصَلُّوا إِلَيْهَا».
Amekataza -Rehema na amani ziwe juu yake- kukaa juu ya makaburi. Kama alivyokataza kusali kwa kuyaelekea makaburi, kwa kaburi kuwa upande wa kibla cha mwenye kusali; kwa sababu hilo ni katika njia za shirki.
Katazo la kusali makaburini au kati kati yake au kuyaelekea, isipokuwa swala ya jeneza kama ilivyothibiti katika mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Katazo la kusali kwa kuyaelekea makaburi ni kuziba mianya ya kuingia katika ushirikina.
Uislamu umekataa kuchupa mipaka katika makaburi na kuyadhalilisha pia, hakuna kuyapuuza wala kuyatukuza.
Heshima ya muislamu inabakia hata baada ya kufa kwake, kwa kauli yake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kuvunja mfupa wa maiti ni kama kuuvunja akiwa hai".
Swahiih Muslim (2/ 668) (972).
Zaidi (6)
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام.
لعبد الله البسام (2/ 30).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام.
لمحمد العثيمين (1/ 522).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام.
لعبد الله الفوزان (4/ 285).