Skip to content

Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni walioko ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni

Imepokewa Kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:

"Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni walioko ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni."

«الرَّاحِمُونَ يَرْحَمُهمُ الرَّحمنُ، ارحَمُوا أهلَ الأرضِ يَرْحْمْكُم مَن في السّماء».

Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad
Sahihi
Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wale wenye kuwahurumia wenzao huwahurumia Rahman -Mwingi wa rehema- kwa huruma yake iliyokienea kila kitu; Yakiwa ni malipo sawa na matendo yao. Kisha akaamrisha -Rehema na amani ziwe juu yake-kuwahurumia wote walioko ardhini kwanzia binadamu au wanyama au ndege, au wengineo katika aina ya viumbe mbali mbali, na malipo ya hilo; mtahurumiwa na Mwenyezi Mungu kutoka juu ya mbingu yake ya saba.

Maana ya Maneno

...:

Katika Faida za Hadithi

Dini ya Uislamu ni dini ya huruma, na dini nzima imesimama katika kumtii Mwenyezi Mungu na kuwatendea wema viumbe.

Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka anasifika kwa sifa ya huruma, naye Mtukufu ni Mwingi wa rehema mwenye kurehemu, mfikishaji wa huruma kwa waja wake.

Malipo huendana na matendo, wenye huruma huwahurumia Rahman -Mwingi wa rehema-.

Rejea

Sunanu Abii Daud (7/ 297) (4941).

Sunanu Tirmidhiy (3/ 483) (1924).

Zaidi (7)

مسند أحمد ط الرسالة (11/ 33) (6494).

تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي.

لمحمد المباركفورى (6/ 43).

سلسلة الأحاديث الصحيحة وشيء من فقهها وفوائدها.

للألباني (2/ 594).

معارج القبول بشرح سلم الوصول إلى علم الأصول.

حافظ الحكمي (1/ 156).