Sharti zenye haki zaidi kwenu nyinyi kuzitekeleza ni zile mlizohalalishia tupu
Imepokewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake:
"Sharti zenye haki zaidi kwenu nyinyi kuzitekeleza ni zile mlizohalalishia tupu".
«أَحَقُّ الشُّرُوطِ أَنْ تُوفُوا بِهِ مَا اسْتَحْلَلْتُمْ بِهِ الْفُرُوجَ».
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa sharti bora kabisa kwa kutekelezwa ni zile zilizokuwa sababu ya uhalali wa kustarehe na mwanamke, nazo ni zile sharti za halali anazozitaka mwanamke wakati wa kufunga ndoa.
...:
Uwajibu wa kutekeleza sharti ambazo amezitilia umuhimu mmoja kati ya wanandoa wawili kwa mwenzie, isipokuwa sharti itakayoharamisha halali au kuhalalisha haramu.
Kutekeleza sharti za ndoa kumetiliwa mkazo kuliko sharti zote; kwa sababu huambatana na kuhalalisha tupu.
Ukubwa wa nafasi ya ndoa katika Uislamu, kiasi ambacho umetilia mkazo juu ya kutimiza sharti zake.
Swahiih Al Bukhaariy (3/ 190) (2721).
Swahiih Muslim (2/ 1035) (1418).
Zaidi (4)
الإلمام بشرح عمدة الأحكام.
لإسماعيل الأنصاري (2/ 63).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام.
لعبد الله البسام (ص573).