Skip to content

Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio

Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema:

"Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio".

«مَنِ اسْتَطَاعَ البَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ، فَإِنَّهُ أَغَضُّ لِلْبَصَرِ، وَأَحْصَنُ لِلْفَرْجِ، وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ، فَإِنَّهُ لَهُ وِجَاءٌ».

Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
Sahihi
Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amewahimiza wenye uwezo wa tendo la ndoa na gharama ya ndoa waoe; kwani hilo Iinahifadhi macho yake kutokana na mambo yaliyokatazwa, linalinda usafi wake wa mwili, na linamzuia asiingie katika uasherati, ambaye hawezi kukidhi mahitaji ya ndoa hali ya kuwa ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa basi ni lazima afunge, kwani hii itakata matamanio ya tupu na shari ya manii.

Katika Faida za Hadithi

Uislamu umechunga sana sababu za mtu kujizuia na machafu na kusalimika na machafu.

Himizo la kufunga swaum kwa ambaye hatoweza gharama za ndoa; kwa sababu hudhoofisha matamanio.

Kufunga kunafananishwa na kuhasiwa; Kwa sababu kuhasi ni kuchubua mishipa ya korodani mbili, na kwa kitendo hicho hupotea matamani ya tendo la ndoa, hivyo hivyo swaumu hudhoofisha hamu ya tendo la ndoa.

Rejea

Swahiih Al Bukhaariy (3/ 26) (1905).

Swahiih Muslim (2/ 1018) (1400).

Zaidi (6)

الإلمام بشرح عمدة الأحكام للشيخ.

لإسماعيل الأنصاري (2/ 57).

تيسير العلام شرح عمدة الأحكام.

لعبد الله البسام (ص565).

خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام.

لفيصل آل مبارك (ص281).