Skip to content

Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:

"Atakayempa muda mwenye hali ngumu, au akamfutia deni, Allah atampa kivuli siku ya kiyama chini ya kivuli cha Arshi yake siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake."

«مَنْ أَنْظَرَ مُعْسِرًا، أَوْ وَضَعَ لَهُ، أَظَلَّهُ اللهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ تَحْتَ ظِلِّ عَرْشِهِ يَوْمَ لَا ظِلَّ إِلَّا ظِلُّهُ».

Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
Sahihi
Ufafanuzi

Ametueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayempa muda mdaiwa wake au akampunguzia katika deni lake, basi malipo yake: Nikuwa Allah atampa kivuli siku ya Kiyama ambayo jua litasogea karibu na vichwa vya waja na joto lake litakuwa kali mno, Hatopata yeyote kivuli isipokuwa atakayetiwa kivuli na Mwenyezi Mungu.

Maana ya Maneno

عرشه: العرش هو المخلوق العظيم الذي استوى عليه الرحمن، ولا يقدر قدرَه إلا الله عز وجل.

Katika Faida za Hadithi

Fadhila za kuwafanyia wepesi waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa hilo ni katika sababu za kuokoka na misukosuko ya siku ya Kiyama.

Malipo huenda sawa na matendo.

Rejea

Sunanu Tirmidhiy (2/ 575) (1306).

Musnad wa Ahmad (14/ 329) (8711).

Zaidi (8)

كنوز رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (16/ 412).

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.

لسليم الهلالي (2/ 459).

فيض القدير شرح الجامع الصغير.

للمناوي (6/ 89).

نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.

لمجموعة من الباحثين (2/ 947).