Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu
Kutoka kwa Mus'abu bin Saadi amesema: Alijiona Saadi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana thamani kuliko aliye chini yake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu".
«هَلْ تُنْصَرُونَ وَتُرْزَقُونَ إِلَّا بِضُعَفَائِكُمْ».
Alidhania Saadi bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana ubora kuliko aliye chini yake katika watu madhaifu, kwa sababu ya ushujaa wake na mfano wa hilo!. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Tambueni kuwa hamnusuriwi wala hampewi riziki isipokuwa kwa watu wenu madhaifu kwa dua zao na swala zao na utakasifu wao wa nia; kwani wao mara nyingi ndio hutakasa dua zaidi, na huwa na unyenyekevu zaidi katika ibada kwa sababu nyoyo zao ziko tupu hazifungamani na mapambo ya dunia.
Himizo la kuwa mnyenyekevu na katazo la kujiona bora kwa watu wengine.
Amesema bin Hajari: Ikiwa mwenye nguvu anakuwa na hadhi kwa ubora wa ushujaa wake, basi mtu dhaifu anakuwa bora kwa dua yake na utakasifu wa nia yake (Ikhlas yake).
Himizo la kutenda wema kwa mafakiri na kuwapa haki zao, kwani hilo ni katika sababu za kupata rehema ya Mwenyezi Mungu kwako na msaada wake.
Swahiih Al Bukhaariy (4/ 36) (2896).
Zaidi (6)
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين.
لسليم الهلالي (1/ 354).
شرح رياض الصالحين.
لابن عثيمين (3/ 111).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين.
لمجموعة من الباحثين (1/ 279).
Imenukuliwa katika vitabu
5 VitabuZaidi (5)
- رياض الصالحينرياض الصالحين مع فوائد وهدايات - 2«هَلْ تُنْصَرُونَ وَتُرْزَقُونَ إلَّا بِضُعَفَائِكُمْ».
- مجالس تدارس القرآن للمبتدئين (سورة الفاتحة وقصار المفصّل)1«هل تنصرون وترزقون إلا بضعفائكم»([101]).
- مجموعة زاد الحديث(3)1«هَلْ تُنْصَرُونَ وَتُرْزَقُونَ إِلَّا بِضُعَفَائِكُم؟!»
- مجموعة زاد الحديث(3)1«هَلْ تُنْصَرُونَ وَتُرْزَقُونَ إِلَّا بِضُعَفَائِكُمْ؟!»
- نبراس طالب (2)نبراس طالب (2) «هَلْ تُنْصَرُونَ وَتُرْزَقُونَ إِلَّا بِضُعَفَائِكُمْ؟»