Skip to content
Al-Anfal /

Aya 75

8 : 75

Aya 75 of Al-Anfal (8 : 75). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Anfal Aya 75
Sura · Al-Anfal
Kiswahili · Barawani
8 : 75

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنۢ بَعۡدُ وَهَاجَرُواْ وَجَٰهَدُواْ مَعَكُمۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ مِنكُمۡۚ وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ

Na watakao amini baadaye na wakahajiri, na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi hao ni katika nyinyi. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na walio amini baada ya wale wa mwanzo, na mwishoe wakahama nao, na wakapigana Jihadi pamoja na walio tangulia, basi hao ni katika nyinyi, kwa mkusanyiko wa Muhaajirina (Walio hama Makka) na Ansari (walio msaidia Mtume, watu wa Madina). Hao wanastahiki ulinzi na haki kama ziliopo baina ya nyinyi kwa nyinyi. Na walio kuwa wame nasibiana katika Waumini - juu ya urafiki wa Imani -wana urafiki zaidi wa kuwa ni jamaa. Basi hao wanazidiana katika mapenzi, na mali, na kusaidiana, na kuungana mkono. Na Mwenyezi Mungu ameyabainisha hayo katika Kitabu chake. Naye ni Mwenye kujua kila kitu.