Skip to content
الأنفَال /

Aya 71

8 : 71

Aya 71 of الأنفَال (8 : 71). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنفَال Aya 75
Sura · الأنفَال
Kiswahili · Barawani
8 : 71

وَإِن يُرِيدُواْ خِيَانَتَكَ فَقَدۡ خَانُواْ ٱللَّهَ مِن قَبۡلُ فَأَمۡكَنَ مِنۡهُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Ikiwa wanataka kukufanyia khiana, wao walikwisha mfanyia khiana Mwenyezi Mungu kabla yake, na Yeye akakuwezesha kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Na pindi wakitaka kukukhuni, kwa vile baadhi yao walivyo onyesha kumili kwenye Uislamu, pamoja na nyoyo zao kupenda kukufanyia khiana makusudi, wewe usivunjike moyo. Mwenyezi Mungu atakupa uwezo juu yao. Kama hapo kwanza walipo mkhini Mwenyezi Mungu kwa kumfanyia wenzi na washirika wa kuwaabudu, na wakaikufuru neema yake, na Yeye aliwaweza kwa kukupa ushindi juu yao katika Badri, juu ya kuwa jeshi lako ni dogo na lao ni kubwa. Na Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye ushindi, Muendeshaji kwa hikima yake, aliwathibitisha wakawa na nguvu waja wake Waumini kwa nusura yake.