Skip to content
الأنفَال /

Aya 6

8 : 6

Aya 6 of الأنفَال (8 : 6). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنفَال Aya 75
Sura · الأنفَال
Kiswahili · Barawani
8 : 6

يُجَٰدِلُونَكَ فِي ٱلۡحَقِّ بَعۡدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى ٱلۡمَوۡتِ وَهُمۡ يَنظُرُونَ

Wanajadiliana nawe kwa jambo la Haki baada ya kwisha bainika, kama kwamba wanasukumwa kwenye mauti nao wanaona.

Explanation & meanings · 1
  1. Wanajadiliana nawe hao wa kikundi hicho, na wanajaribu kutilia nguvu kauli yao katika jambo la haki, nalo ni kutoka kwa ajili ya Jihadi. Na kumbe wao walikuwa na wenzao walio toka kwenda kupokonya mali ya Makureshi yaliyo kuwa yanakwenda Sham, na wasiyapate. Kikundi hichi kikakhiari kurejea baada ya kuona wamenusurika, kwa kujuvywa na Mtume, na kwamba makafiri wanawaogopa, na kwa kuwa hadi wakivichukia vita, na kuwa hawajui litalo wapata. Na walipo kuwa wakiviendea vita walikuwa kama wanao sukumwa kwenda kufa, na wao wanaona kitacho wauwa, na yanawapata mateso yake.