Skip to content
الأنفَال /

Aya 29

8 : 29

Aya 29 of الأنفَال (8 : 29). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنفَال Aya 75
Sura · الأنفَال
Kiswahili · Barawani
8 : 29

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَتَّقُواْ ٱللَّهَ يَجۡعَل لَّكُمۡ فُرۡقَانٗا وَيُكَفِّرۡ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلۡفَضۡلِ ٱلۡعَظِيمِ

Enyi mlio amini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atakupeni kipambanuo, na atakufutieni makosa, na atakusameheni, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi mlio isadiki Haki na mkaifuata! Mkizinyenyekea amri za Mwenyezi Mungu kwa siri na dhaahiri, Mwenyezi Mungu atakujaalieni katika nafsi zenu uwezo wa kupambanua baina ya Haki na upotovu, na atakutunukieni ushindi wa kutenga baina yenu na maadui zenu, na atakusitirieni maovu yenu yaondoke, naye akusameheni. Na Yeye Subhanahu daima ni Mwenye fadhila kubwa.