Skip to content
الطَّلَاق /

Aya 11

65 : 11

Aya 11 of الطَّلَاق (65 : 11). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الطَّلَاق Aya 12
Sura · الطَّلَاق
Kiswahili · Barawani
65 : 11

رَّسُولٗا يَتۡلُواْ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ مُبَيِّنَٰتٖ لِّيُخۡرِجَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۚ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعۡمَلۡ صَٰلِحٗا يُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ قَدۡ أَحۡسَنَ ٱللَّهُ لَهُۥ رِزۡقًا

Mtume anaye kusomeeni Aya za Mwenyezi Mungu zinazo bainisha, ili kuwatoa walio amini na wakatenda mema kutoka gizani kuwapeleka kwenye nuru. Na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na akatenda mema, atamwingiza katika Bustani zipitazo mito kati yake, wadumu humo milele. Mwenyezi Mungu amekwisha mpa riziki nzuri.

Explanation & meanings · 1
  1. Mtume anaye kusomeeni Aya za Mwenyezi Mungu zenye kukubainishieni baina yaliyo kweli na ya uwongo, ili awatoe walio amini na wakatenda mema kutoka kwenye giza la upotovu kwenda kwenye mwangaza wa hidaya. Na mwenye kumsadiki Mwenyezi Mungu, na akatenda vitendo vyema atamtia katika Bustani zinazo pita kati yake mito. Watakaa humo milele. Mwenyezi Mungu kamfanyia ihsani Muumini mwema kwa kumpa riziki iliyo njema.