Skip to content
الأنعَام /

Aya 88

6 : 88

Aya 88 of الأنعَام (6 : 88). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 88

ذَٰلِكَ هُدَى ٱللَّهِ يَهۡدِي بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۚ وَلَوۡ أَشۡرَكُواْ لَحَبِطَ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo humhidi amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Hiyo ndiyo tawfiqi kubwa waliyo ipata watu hawa, nayo ni tawfiqi (uwezesho) iliyo tokana na Mwenyezi Mungu, ambayo humwafiqia (humwezesha) amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli shiriki watu hawa walio khitariwa zingeli potea a'mali zao za kheri zote walizo zifanya, na wasingeli pata thawabu.