Skip to content
الأنعَام /

Aya 140

6 : 140

Aya 140 of الأنعَام (6 : 140). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 140

قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ قَتَلُوٓاْ أَوۡلَٰدَهُمۡ سَفَهَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ٱفۡتِرَآءً عَلَى ٱللَّهِۚ قَدۡ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ

Hakika wamekhasirika wale ambao wamewauwa watoto wao kwa upumbavu pasipo kujua, na wakaharimisha alivyo waruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu. Hakika wamepotea, wala hawakuwa wenye kuongoka.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika wamekhasiri hao walio wauwa watoto wao kwa ujinga na kwa mawazo ya uwongo, bila ya kujua nini matokeo ya kitendo chao, wala sababu yake; na wakajiharimishia nafsi zao riziki alizo waruzuku Mwenyezi Mungu katika mimea, na wanyama, huku wakimzulia Mwenyezi Mungu kwa kudai kuwa ni Yeye ndiye aliye harimisha. Na hakika wamejitenga mbali na Haki kwa sababu hiyo. Na kwa sababu ya uzushi huu hawakuwa katika wanao sifika kwa uwongofu.