Skip to content
الأنعَام /

Aya 130

6 : 130

Aya 130 of الأنعَام (6 : 130). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 130

يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي وَيُنذِرُونَكُمۡ لِقَآءَ يَوۡمِكُمۡ هَٰذَاۚ قَالُواْ شَهِدۡنَا عَلَىٰٓ أَنفُسِنَاۖ وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ

Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia Siku ya Kiyama: Enyi watu na majini! Mitume wamekujieni wakikutajieni hoja na dalili zilizo wazi, na wakikusomeeni Aya, na wakikuonyeni na mkutano wa Mwenyezi Mungu katika Siku yenu hii. Basi vipi mnakanusha? Nao watajibu: Tunakubali wenyewe madhambi tuliyo yatenda. Na maisha ya kidunia yaliwakhadaa kwa starehe zake, na wakajikiria nafsi zao kuwa hakika wao walikuwa wapinzani.