Skip to content
الأنعَام /

Aya 104

6 : 104

Aya 104 of الأنعَام (6 : 104). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 104

قَدۡ جَآءَكُم بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡۖ فَمَنۡ أَبۡصَرَ فَلِنَفۡسِهِۦۖ وَمَنۡ عَمِيَ فَعَلَيۡهَاۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِحَفِيظٖ

Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa faida yake mwenyewe, na anaye pofuka basi ni khasara yake. Nami si mtunzaji wenu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Waambie watu: Zimekwisha kujieni kutoka kwa Muumba wenu na Mwenye kumiliki mambo yenu yote, hoja na maelezo wazi katika hii Qur'ani. Hizo zinakuangazieni Njia ya Haki. Basi mwenye kunafiika kwazo, manufaa ni yake mwenyewe. Na mwenye kujitenga nazo, basi amejidhuru mwenyewe! Wala mimi si mlinzi wenu, bali mimi ni Mjumbe ninakufikishieni niliyo tumwa kwenu.