Skip to content
الحَشر /

Aya 18

59 : 18
الحَشر Aya 24
Sura · الحَشر
Kiswahili · Barawani
59 : 18

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡتَنظُرۡ نَفۡسٞ مَّا قَدَّمَتۡ لِغَدٖۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kila nafsi iangalie inayo yatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi mlio amini! Jiwekeeni kinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kujilazimisha kumt'ii Yeye. Na kila nafsi izingatie a'mali gani ya kuikadimisha kwa ajili ya Kesho. Na jilazimisheni kumcha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari vilivyo kwa yote myatendayo. Naye atakulipeni kwa hayo.