Skip to content
المَائدة /

Aya 20

5 : 20

Aya 20 of المَائدة (5 : 20). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 20

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ جَعَلَ فِيكُمۡ أَنۢبِيَآءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكٗا وَءَاتَىٰكُم مَّا لَمۡ يُؤۡتِ أَحَدٗا مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu, alipo wateuwa Manabii kati yenu, na akakufanyeni watawala, na akakupeni ambayo hakuwapa wowote katika walimwengu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na taja, ewe Mtume! pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu kwa kushukuru na kut'ii, kwa kuwa amewateua Manabii wengi miongoni mwenu, na akakufanyeni watukufu kama wafalme baada ya kuwa mlikuwa wanyonge chini ya utawala wa Firauni, na akakupeni neema nyingi nyenginezo ambazo hawajapewa wowote wengineo.