Skip to content
المَائدة /

Aya 109

5 : 109

Aya 109 of المَائدة (5 : 109). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 109

۞ يَوۡمَ يَجۡمَعُ ٱللَّهُ ٱلرُّسُلَ فَيَقُولُ مَاذَآ أُجِبۡتُمۡۖ قَالُواْ لَا عِلۡمَ لَنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّٰمُ ٱلۡغُيُوبِ

Ile siku ambayo Mwenyezi Mungu atapo wakusanya Mitume awaambie: Mlijibiwa nini? Watasema: Hatuna ujuzi; hakika Wewe ndiye Mjuzi Mkubwa wa yote yaliyo fichikana.

Explanation & meanings · 1
  1. Nanyi ikumbukeni Siku ya Kiyama pale Mwenyezi Mungu atapo wakusanya mbele yake Mitume wote akawauliza: Hao kaumu zenu niliyo kutumeni kwao wamekujibuni nini? Waliamini au walikanya? Na hao kaumu wakati huo watakuwa wamehudhuria ili hoja iwe juu yao kwa ushahidi wa Mitume wao wakisema: Hakika sisi hatujui yaliyo tokea baada yetu kwa hao ulio tupeleka kwao. Ni Wewe peke yako ndiye unaye jua hayo, kwa kuwa Wewe ndiye uliye kusanya ujuzi wa vilivyo fichikana kama unavyo jua viliyo dhaahiri.