46 : 33
أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّ ٱللَّهَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَلَمۡ يَعۡيَ بِخَلۡقِهِنَّ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧيَ ٱلۡمَوۡتَىٰۚ بَلَىٰٓۚ إِنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Je! Hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliye ziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu? Kwani? Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Explanation & meanings · 1
- Wameghafilika wala hawajui kwamba Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi, na wala hakushindwa kuziumba, ni Muweza wa kuwafufua maiti? Bali Yeye ni Muweza wa hayo, kwani Yeye Mtukufu ana uweza kaamili juu ya kila kitu.