Skip to content
الأحقَاف /

Aya 26

46 : 26

Aya 26 of الأحقَاف (46 : 26). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأحقَاف Aya 35
Sura · الأحقَاف
Kiswahili · Barawani
46 : 26

وَلَقَدۡ مَكَّنَّٰهُمۡ فِيمَآ إِن مَّكَّنَّٰكُمۡ فِيهِ وَجَعَلۡنَا لَهُمۡ سَمۡعٗا وَأَبۡصَٰرٗا وَأَفۡـِٔدَةٗ فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُمۡ سَمۡعُهُمۡ وَلَآ أَبۡصَٰرُهُمۡ وَلَآ أَفۡـِٔدَتُهُم مِّن شَيۡءٍ إِذۡ كَانُواْ يَجۡحَدُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Na bila ya shaka tuliwaweka vizuri sio kama tulivyo kuwekeni nyinyi; na tuliwapa masikio, na macho, na nyoyo. Na hayakuwafaa kitu masikio yao, wala macho yao, wala nyoyo zao kwa lolote. Kwani hao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu, na yale waliyo kuwa wakiyafanyia maskhara ndiyo yakawazunguka.

Explanation & meanings · 1
  1. Na tuliwaweka kabila la A'di kwa nafasi na nguvu sio kama tulivyo kuwekeni nyinyi watu wa Makka. Na tuliwajaalia masikio, na macho, na nyoyo, lau wangeli taka kunafiika kwayo. Lakini hayakuwafaa hata kitu kidogo masikio yao, wala macho yao, wala nyoyo zao, kwa sababu walikuwa wakizikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu. Basi hayo yakapinga baina yao na kunafiika kwa waliyo letewa. Na ile ile adhabu waliyo kuwa wakiifanyia maskhara ikawazunguka.