Skip to content
النِّسَاء /

Aya 93

4 : 93

Aya 93 of النِّسَاء (4 : 93). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 93

وَمَن يَقۡتُلۡ مُؤۡمِنٗا مُّتَعَمِّدٗا فَجَزَآؤُهُۥ جَهَنَّمُ خَٰلِدٗا فِيهَا وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ وَلَعَنَهُۥ وَأَعَدَّ لَهُۥ عَذَابًا عَظِيمٗا

Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika mwenye kumuuwa Muumini kwa mauwaji ya kukusudia na kuona ndio ndivyo mauwaji hayo, Jaza yake inayo lingana na ukhalifu huo ni kuingizwa Motoni milele, na kughadhibikiwa na Mwenyezi Mungu na afukuzwe kutokana na rehema yake. Na Mwenyezi Mungu amemtengezea Akhera adhabu kubwa, kwani kitendo hichi ndio ukhalifu mkubwa kabisa katika dunia.