Skip to content
النِّسَاء /

Aya 89

4 : 89

Aya 89 of النِّسَاء (4 : 89). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 89

وَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ كَمَا كَفَرُواْ فَتَكُونُونَ سَوَآءٗۖ فَلَا تَتَّخِذُواْ مِنۡهُمۡ أَوۡلِيَآءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَخُذُوهُمۡ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ وَجَدتُّمُوهُمۡۖ وَلَا تَتَّخِذُواْ مِنۡهُمۡ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرًا

Wanapenda lau kuwa nanyi mnge kufuru kama walivyo kufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msiwafanye marafiki miongoni mwao mpaka wahame kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu. Na wakikengeuka basi wakamateni na wauweni popote mnapo wapata. Wala msimfanye rafiki katika wao wala msaidizi.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika nyinyi mnapenda kuwaongoa hawa wanaafiki, na wao wanapenda nyinyi mkufuru kama wao, ili muwe nyote sawa kwa ukafiri. Ilivyo kuwa hivyo basi msitake wa kukuungeni mkono miongoni mwao. Wala msiwafanye wenzenu, mpaka wakubali kutoka huko kwao kuwania Jihadi kwa ajili ya Uislamu. Hivyo tu ndio itawatoka sifa ya unaafiki. Lakini wakiyakataa hayo, wakaungana na maadui zenu, basi wauweni popote mtapo wapata, wala msiwaone kuwa ni wenzenu, wala msiwachukulie kuwa ndio wasaidizi wenu.