Skip to content
النِّسَاء /

Aya 63

4 : 63

Aya 63 of النِّسَاء (4 : 63). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 63

أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعۡلَمُ ٱللَّهُ مَا فِي قُلُوبِهِمۡ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَعِظۡهُمۡ وَقُل لَّهُمۡ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَوۡلَۢا بَلِيغٗا

Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali, uwape mawaidha na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.

Explanation & meanings · 1
  1. Hao ndio wanao kula yamini kuwa hawakutaka ila wema na vitendo vya muwafaka. Mwenyezi Mungu anayajua vyema yaliyomo katika nyoyo zao, na anaujua uwongo wa hiyo kauli yao. Basi wewe usishughulike na maneno yao. Waite kwenye haki kwa mawaidha yaliyo mema, na sema nao maneno yenye hikima yenye kuathiri yanayo fika ndani ya nyoyo zao.