Skip to content
النِّسَاء /

Aya 18

4 : 18

Aya 18 of النِّسَاء (4 : 18). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 18

وَلَيۡسَتِ ٱلتَّوۡبَةُ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ إِنِّي تُبۡتُ ٱلۡـَٰٔنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمۡ كُفَّارٌۚ أُوْلَٰٓئِكَ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا

Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanao kufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu.

Explanation & meanings · 1
  1. Toba isiyo kubaliwa ni ya wanao fanya maasi kisha hawafanyi haraka kuyajutia mpaka mmoja afikwapo na mauti. Tena hapo husema: Sasa mimi natangaza majuto na toba. Kadhaalika toba haikubaliwi kutokana na wanao kufa katika ukafiri. Mwenyezi Mungu ameyaandalia makundi mawili hayo adhabu ya kutia uchungu huko kwenye nyumba ya malipo, Akhera.