Skip to content
An-Nisa /

Aya 17

4 : 17

Aya 17 of An-Nisa (4 : 17). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

An-Nisa Aya 176
Sura · An-Nisa
Kiswahili · Barawani
4 : 17

إِنَّمَا ٱلتَّوۡبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٖ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika toba imedhaminiwa na Mwenyezi Mungu kwa watendao maovu katika hali ya ujinga, na kupitikiwa na kutoangalia vyema, kisha wakafanya haraka ya kutubu kabla ya kufikiwa na mauti. Hawa basi Mwenyezi Mungu anaikubali toba yao, naye ni Mjuzi, haumfichikii ukweli wa toba, ni Mwenye hikima, hakosei katika kupima.