Skip to content
النِّسَاء /

Aya 173

4 : 173
النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 173

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَيُوَفِّيهِمۡ أُجُورَهُمۡ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضۡلِهِۦۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسۡتَنكَفُواْ وَٱسۡتَكۡبَرُواْ فَيُعَذِّبُهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا

Na ama walio amini na wakatenda mema atawalipa ujira wao sawa sawa, na atawazidishia kwa fadhila yake. Na ama wale walio ona uvunjifu na wakafanya kiburi, basi atawaadhibu adhabu iliyo chungu. Wala hawatopata mlinzi wala wa kuwanusuru asiye kuwa Mwenyezi Mungu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ama walio amini wakatenda mema atawalipa thawabu za vitendo vyao, na atawazidishia kwa fadhila yake, kwa kuwakirimu na kuwaneemesha. Na ama wale walio kataa kumuabudu, na wakajiona bora wasimshukuru, hao amewaandalia adhabu yenye machungu makali. Hapana msaidizi wa kuwakinga nayo wala wa kuwanusuru.