Skip to content
An-Nisa /

Aya 154

4 : 154

Aya 154 of An-Nisa (4 : 154). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

An-Nisa Aya 176
Sura · An-Nisa
Kiswahili · Barawani
4 : 154

وَرَفَعۡنَا فَوۡقَهُمُ ٱلطُّورَ بِمِيثَٰقِهِمۡ وَقُلۡنَا لَهُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا وَقُلۡنَا لَهُمۡ لَا تَعۡدُواْ فِي ٱلسَّبۡتِ وَأَخَذۡنَا مِنۡهُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا

Na tukanyanyua mlima juu yao kwa kufanya agano nao. Na tukawaambia: Ingilieni mlangoni kwa unyenyekevu. Na tukawaambia: Msiivunje Siku ya Sabato (Jumaa mosi). Na tukachukua kwao ahadi iliyo madhubuti.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu akaunyanyua mlima juu ya Wana wa Israili ili kuwatisha kwa kule kuikataa kwao sharia ya Taurati, mpaka wakaikubali. Akachukua kwao agano, na akawaamrisha waingie mjini hali wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Wala wasiyakiuke aliyo waamrisha kushika ibada katika siku ya Sabato, yaani Jumaamosi.(Imeitwa "Sabt" Kiarabu, "Shabbath" Kiyahudi, "Sabbath" Kiingereza, na "Sabato" Kiswahili, maana yake "Mapumziko" kwa kuwa ni siku ya mapumziko kwa Mayahudi.) Na Mwenyezi Mungu alichukua kwao ahadi ya nguvu.