Skip to content
An-Nisa /

Aya 126

4 : 126

Aya 126 of An-Nisa (4 : 126). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

An-Nisa Aya 176
Sura · An-Nisa
Kiswahili · Barawani
4 : 126

وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٖ مُّحِيطٗا

Ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuvizunguka vitu vyote.

Explanation & meanings · 1
  1. Hakika wa kumtakasia niya ni Mwenyezi Mungu, na ndio kwake Yeye inapasa uusilimishe uso wako, yaani umuelekee na umnyenyekee. Huko ndiko kumsafia niya Mwenyezi Mungu aliye umba ulimwengu wote, na ndiye mwenye kuumiliki. Vitu vyote viliomo mbinguni na duniani - nyota, sayari, jua, mwezi, milima, mabonde, majangwa, mashamba n.k. ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kubainikiwa na kila kitu, Mwenye kujua kwa ujuzi mkamilifu wa kuvizunguka vitu vyote avitendavyo mwanaadamu. Na Yeye atamlipa kheri akitenda kheri, na shari akitenda shari.