Skip to content
الأحزَاب /

Aya 24

33 : 24

Aya 24 of الأحزَاب (33 : 24). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأحزَاب Aya 73
Sura · الأحزَاب
Kiswahili · Barawani
33 : 24

لِّيَجۡزِيَ ٱللَّهُ ٱلصَّٰدِقِينَ بِصِدۡقِهِمۡ وَيُعَذِّبَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ إِن شَآءَ أَوۡ يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا

Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa sababu ya ukweli wao, na awaadhibu wanaafiki pindi akitaka, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Explanation & meanings · 1
  1. Ili Mwenyezi Mungu apate kuwalipa Waumini walio wakweli kwa sababu ya ukweli wao katika Imani yao na kutimiza kwao ahadi waliyo itoa. Na awaadhibu wanaafiki - pindi akitaka - au amwezeshe aliye elekea, kufikia toba. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe kwa kukubali toba, Mwenye kurehemu kwa kusamehe maasi.