33 : 17
قُلۡ مَن ذَا ٱلَّذِي يَعۡصِمُكُم مِّنَ ٱللَّهِ إِنۡ أَرَادَ بِكُمۡ سُوٓءًا أَوۡ أَرَادَ بِكُمۡ رَحۡمَةٗۚ وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا
Sema: Ni nani wa kukulindeni na Mwenyezi Mungu pindi akikutakieni uovu, au akikutakieni rehema? Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
Explanation & meanings · 1
- Waambie hawa wanao babaika: Nani atakaye kulindeni na Mwenyezi Mungu akitaka kukuleteeni shari, au atakaye kuzuieni msipate kheri, akitaka Yeye kukurehemuni? Wala hawatapata badala ya Mwenyezi Mungu yeyote wa kuwalinda au kuwaokoa.