Skip to content
الرُّوم /

Aya 40

30 : 40

Aya 40 of الرُّوم (30 : 40). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الرُّوم Aya 60
Sura · الرُّوم
Kiswahili · Barawani
30 : 40

ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ ثُمَّ رَزَقَكُمۡ ثُمَّ يُمِيتُكُمۡ ثُمَّ يُحۡيِيكُمۡۖ هَلۡ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَفۡعَلُ مِن ذَٰلِكُم مِّن شَيۡءٖۚ سُبۡحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ

Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, kisha akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote katika hao mnao washirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka na hayo mnayo mshirikisha naye.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu Subhaanu Alietakasaika, ndie aliekuumbeni, kisha kakupeni cha kukupeeni maisha, kisha ndie anaekufesheni, na kisha atakufufueni kutoka makaburini mwenu. Je? Yupo yoyote katika hao miungu ya kishirikina mnao dai na mukaawabudu badala ya Mwenyezi Mungu mwenye kutenda hayo ya kuumba na kukuruzuku, na kufisha na kukufua, au kitendo chochote, Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo wanao mshirikisha naye.