28 : 9
وَقَالَتِ ٱمۡرَأَتُ فِرۡعَوۡنَ قُرَّتُ عَيۡنٖ لِّي وَلَكَۖ لَا تَقۡتُلُوهُ عَسَىٰٓ أَن يَنفَعَنَآ أَوۡ نَتَّخِذَهُۥ وَلَدٗا وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Na mkewe Firauni alisema: Atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu. Wala wao hawakutambua.
Explanation & meanings · 1
- Mke wa Firauni alipo mwona mtoto alimwambia mumewe: Mtoto huyu atatuletea furaha mimi na wewe. Tumweke, tusimuuwe, kwa kutaraji kuwa atakuja tufaa kuendesha mambo yetu. Au tumfanye mwenetu wa kumlea. Na wao kumbe hawatambui aliyo mkadiria Mwenyezi Mungu.