Skip to content
Al-Qasas /

Aya 80

28 : 80

Aya 80 of Al-Qasas (28 : 80). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Qasas Aya 88
Sura · Al-Qasas
Kiswahili · Barawani
28 : 80

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ وَيۡلَكُمۡ ثَوَابُ ٱللَّهِ خَيۡرٞ لِّمَنۡ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗاۚ وَلَا يُلَقَّىٰهَآ إِلَّا ٱلصَّٰبِرُونَ

Na wakasema wale walio pewa ilimu: Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni bora kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Wala hawatapewa hayo isipo kuwa wenye subira.

Explanation & meanings · 1
  1. Ama wale ambao Mwenyezi Mungu amewaruzuku ilimu yenye manufaa hawakusalitika na hayo. Wakawaelekea walio danganyika kwa kuwanasihi wakiwaambia: Msiyatamani haya, wala msiiache Dini. Kwani yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ya thawabu na neema ni safi zaidi kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Na hiyo ni nasiha ya kweli ambayo hawaikubali ila wenye kuzipiga jihadi nafsi zao, na wakasubiri katika ut'iifu.