28 : 65
وَيَوۡمَ يُنَادِيهِمۡ فَيَقُولُ مَاذَآ أَجَبۡتُمُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na siku atapo waita na akasema: Mliwajibu nini Mitume?
Explanation & meanings · 1
- Na ewe Mtume! Taja vile vile siku washirikina watapo itwa na Mwenyezi Mungu kwa kutahayarishwa, na wakaambiwa: Mliwajibu nini Mitume wangu nilio watuma kwenu wakuiteni kwenye Imani, nao wakafikisha Ujumbe?