28 : 24
فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰٓ إِلَى ٱلظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَآ أَنزَلۡتَ إِلَيَّ مِنۡ خَيۡرٖ فَقِيرٞ
Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayo niteremshia.
Explanation & meanings · 1
- Musa akajitolea kuwakhudumia akawanyweshea. Kisha akenda kuegemea mti akipumzika baada ya kuhangaika kule, naye akisema kwa unyenyekevu: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mwenye haja ya kheri yoyote na riziki yoyote utayo niletea.