Skip to content
القَصَص /

Aya 19

28 : 19

Aya 19 of القَصَص (28 : 19). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

القَصَص Aya 88
Sura · القَصَص
Kiswahili · Barawani
28 : 19

فَلَمَّآ أَنۡ أَرَادَ أَن يَبۡطِشَ بِٱلَّذِي هُوَ عَدُوّٞ لَّهُمَا قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ أَتُرِيدُ أَن تَقۡتُلَنِي كَمَا قَتَلۡتَ نَفۡسَۢا بِٱلۡأَمۡسِۖ إِن تُرِيدُ إِلَّآ أَن تَكُونَ جَبَّارٗا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ مِنَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ

Basi alipo taka kumshika kwa nguvu yule aliye adui wao wote wawili, akasema: Ewe Musa! Unataka kuniuwa kama ulivyo muuwa mtu jana? Wewe hutaki ila kuwa jabari katika nchi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wenye maslaha

Explanation & meanings · 1
  1. Na Musa alipo taka kumtumilia nguvu Mmisri, ambaye ni adui wao wote wawili; kwa sababu ya uadui huu, yule mtu alidhani kuwa Musa atamuuwa, basi akasema: Unataka kuniuwa kama ulivyo muuwa mtu jana? Wewe hutaki ila kuwa muasi tu katika nchi, wala hutaki kuwa miongoni wanao lingania maslaha na kheri.