26 : 50
قَالُواْ لَا ضَيۡرَۖ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ
Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
Explanation & meanings · 1
- Wachawi wakasema: Hapana la kutudhuru sisi kwa adhabu unazo tutishia, kwani sisi ni wenye kurejea kwenye malipo ya Mola wetu Mlezi. Na Yeye ndiye mbora wa kulipa na mbora wa kuadhibu.