26 : 181
۞ أَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَلَا تَكُونُواْ مِنَ ٱلۡمُخۡسِرِينَ
Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja.
Explanation & meanings · 1
- Shuaibu akawaamrisha kutimiza vipimo kwa ukamilifu wanapo pima, kwani ilikuwa ada yao kupunguza kwa pishi na mizani, kupunguza haki za watu kwa kuwapunja na kuwapimia kasoro.