25 : 11
بَلۡ كَذَّبُواْ بِٱلسَّاعَةِۖ وَأَعۡتَدۡنَا لِمَن كَذَّبَ بِٱلسَّاعَةِ سَعِيرًا
Bali wanaikanusha Saa (ya Kiyama). Na Sisi tumemuandalia Moto mkali kabisa huyo mwenye kuikanusha Saa
Explanation & meanings · 1
- Na kwa hakika hawa wamepinga kila Ishara. Kwani wao wamekanusha kufufuliwa, na Siku ya Kiyama. Nao kwa hivyo wanayatia ila matakwa haya ili kuwageuza watu washughulikie upotofu wao. Na Sisi tumekwisha waandalia wanao ikanusha Siku ya Kiyama Moto wenye kuwaka vikali mno.