Skip to content
An-Nur /

Aya 29

24 : 29

Aya 29 of An-Nur (24 : 29). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

An-Nur Aya 64
Sura · An-Nur
Kiswahili · Barawani
24 : 29

لَّيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَدۡخُلُواْ بُيُوتًا غَيۡرَ مَسۡكُونَةٖ فِيهَا مَتَٰعٞ لَّكُمۡۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا تُبۡدُونَ وَمَا تَكۡتُمُونَ

Si vibaya kwenu kuingia nyumba zisio kaliwa ambazo ndani yake yamo manufaa yenu. Na Mwenyezi Mungu anajua mnayo yadhihirisha na mnayo yaficha.

Explanation & meanings · 1
  1. Na mkitaka kuingia nyumba za umma zisio kaliwa na watu makhsusi na ndani yake zipo haja zenu, kama vile maduka, mahoteli, nyumba za ibada, hapana ubaya kuingia bila ya kutaka ruhusa. Na Mwenyezi Mungu anajua kwa ujuzi wa timamu kabisa vitendo vyenu vyote vya dhaahiri na vilivyo fichikana. Basi tahadharini na kwenda kinyume naye.