Skip to content
النور /

Aya 14

24 : 14
النور Aya 64
Sura · النور
Kiswahili · Barawani
24 : 14

وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ لَمَسَّكُمۡ فِي مَآ أَفَضۡتُمۡ فِيهِ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake katika dunia na Akhera, bila ya shaka ingeli kupateni adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyo jiingiza.

Explanation & meanings · 1
  1. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hakukufanyieni fadhila kwa kubainisha hukumu, na hakukurehemuni duniani kwa kuacha kuleta adhabu kwa haraka, na Akhera kwa kukusameheni, angeli kuteremshieni adhabu kubwa kwa sababu ya kujiingiza kwenu katika uzushi huu.