24 : 12
لَّوۡلَآ إِذۡ سَمِعۡتُمُوهُ ظَنَّ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتُ بِأَنفُسِهِمۡ خَيۡرٗا وَقَالُواْ هَٰذَآ إِفۡكٞ مُّبِينٞ
Kwa nini mlipo sikia khabari hii, wanaume Waumini na wanawake Waumini hawakuwadhania wenzao mema, na kusema: Huu ni uzushi dhaahiri?
Explanation & meanings · 1
- Ilikuwa inavyo takikana kwa Imani ni kuwa wakati wa kusikia huu uzushi, ni Waumini wanaume na wanawake wajidhanie nafsi zao kheri ya usafi na unadhifu, na waseme kwa kupinga: Huu ni uwongo ulio wazi umezuliwa, kwa kuwa haya yamemkhusu bora ya Mitume na bora ya wanawake walio wa kweli.