Skip to content
الحج /

Aya 52

22 : 52
الحج Aya 78
Sura · الحج
Kiswahili · Barawani
22 : 52

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ مِن رَّسُولٖ وَلَا نَبِيٍّ إِلَّآ إِذَا تَمَنَّىٰٓ أَلۡقَى ٱلشَّيۡطَٰنُ فِيٓ أُمۡنِيَّتِهِۦ فَيَنسَخُ ٱللَّهُ مَا يُلۡقِي ٱلشَّيۡطَٰنُ ثُمَّ يُحۡكِمُ ٱللَّهُ ءَايَٰتِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii ila anapo soma, Shet'ani hutumbukiza katika masomo yake. Lakini Mwenyezi Mungu huyaondoa anayo yatia Shet'ani; kisha Mwenyezi Mungu huzithibitisha Aya zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Usihuzunike kwa hizi hila za makafiri. Yalimpata kama haya kila Mtume katika Mitume wetu, na kila Nabii katika Manabii wetu. Nayo ni kuwa kila wakiwasomea kitu kwa kuwaita waifuate Haki Mashetani wa kibinaadamu walio asi wakiyapinga ili waubat'ilishe Wito, na wawatie shaka watu kwa yale wanayo somewa. Makusudio yao ni kujiingiza kati baina ya Nabii na matamanio yake ya kutaka Wito wake uitikiwe. Lakini Mwenyezi Mungu huyaondoa wayatakayo. Na mwishoe Haki ndiyo inayo shinda anapo isimamisha Mwenyezi Mungu sharia yake, na akamnusuru Mtume wake. Na Yeye ndiye Mwenye kuzijua hali za watu na vitimbi vyao, Mwenye hikima katika vitendo vyake. Anaweka kila kitu pahala pake.